Wito wa Kutengeneza Nembo ya Hali ya Ramani 2021

Posting this here as volunteer translators did great work translating this OSM blog post to Swahili, but there have been some issues in the communications working group adding it as a new language to the blog platform (which will be fixed soon). Didn’t want the effort to go to waste!

Mwaka 2020, kwa mara ya kwanza tulifanya mkutano wa hali ya ramani mtandaoni! Mwezi Julai mwaka huu, Mkutano huu (SotM 2021) pia utafanyika mtandaoni (tarehe rasimi zitatangazwa katikatu ya mwezi february).

Sura ya SotM ni, kwa kweli, nembo yake: kipengee cha picha kinachotambulika ambacho kinawakilisha uhai na hali ya mkutano wa ulimwengu wa mwaka huo. Kwa sababu hii, tunahitaji msaada wa akili nyingi za ubunifu katika jamii kutengeneza nembo (logo) mpya ya SotM 2021!

State of the Map image

Nembo pia ni muhimu kwa kuelezea muundo na rangi ya tovuti rasmi ya SotM na mtindo wa vitu vilivyomo kwenye mkutano katika majukwaa yote ya OSM. Itatumika pia kwenye vitu tofauti kwenye mkutano kama fulana, stika, nk, na kufanya mkutano uwe na kumbukumbu nzuri zisizisahaulika.

Kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu hadi ubunifu wa kawaida na wapenzi wenye utashi, kila mtu anaweza kushiriki na kutoa mawazo yake kwa jamii!

Mwongozo wa Shindano

Ubunifu wa nembo inapaswa:

  • kuwa mchoro halisi (original)
  • rejea OpenStreetMap (OSM), na State of the Map (SotM)
  • zingatia hisia za jamii ulimwenguni na maadili yake ya msingi
  • kutambulika kwa urahisi
  • leseni ya wazi: CC BY SA au inayohusiana
  • kuwasilishwa Jumapili tarehe 14 Februari 2021 23:59 UTC (03:59 PM EAT)

Jinsi ya kuingia
Tafadhali wasilisha pendekezo lako la nembo kupitia barua pepe kwa sotm@openstreetmap.org, ukiambatanisha faili ya muundo katika fomati ya PNG na muundo wa faili unaoweza kuongezwa au kupunguzwa (kama PDF au SVG).

Uchaguzi wa mshindi
Sanaa/nembo zilizowasilishwa zitakaguliwa na kikundi kinachofanya kazi cha SotM, na nembo ya ushindi itaamuliwa kupitia kura. Nembo rasmi itatangazwa baada ya mkutano wa SotM katikati ya mwezi Februari.

Je unatafuta msukumo au mwangaza?
Angalia logo za mikutano ya SotM iliyopita. Kama una swali lolote, jisikie huru kuwasiliana na kikundi kazi cha SotM kupitia barua pepe: sotm@openstreetmap.org.

Mkutano wa hali ya ramani (State of the Map conference) ni mkutano wa kila mwaka, wa kimataifa wa OpenStreetMap, ulioandaliwa na OpenStreetMap Foundation. OpenStreetMap Foundation ni shirika lisilo la faida, iliyoundwa nchini Uingereza kusaidia Mradi wa OpenStreetMap. Imejitolea kuhamasisha ukuaji, ukuzaji na usambazaji wa data ya kijiografia ya bure/huru kwa kila mtu kutumia na kushiriki. OpenStreetMap Foundation inamiliki na inadumisha miundombinu ya mradi wa OpenStreetMap na unaweza kuiunga mkono kwa kuwa mwanachama.

Kamati ya uandaaji ya State of the Map ni moja katu ya vikundi kazi vyetu vya kijitolea

This post is also available in: English Japanese Spanish Polish